The power of believe on yourself

Dedication: To all girls and women in the world

Kwa majina naitwa Shella Salum nina miaka 33 naishi dar es salaam, Tanzania. Ni mhitimu wa chui kikuu degree of arts with education 2015, Sikupata ajira serikalini nikaajiriwa shule binafsi kama mwalimu nikafundisha kwa miaka 2 toka 2016-2017 ila changamoto ya mwajili wangu alikua hataki likizo yoyote ni kazini mwaka mzima nilipata dharura ya kifamilia nikasafiri kwa wiki mbili kurudi nikafukuzwa kazi.

Iliniumiza ila kwa bahati nikapata sehemu nyingine 2018 -2019 ila tatizo likawa lilelile ni kazi tu hakuna likizo yoyote ila hakuna dharura hata ukipata ugonjwa utapewa siku 2 tu urudi na hapo labda iwe ugonjwa wa kulazwa ila kama ni kawaida utakuja hivo hivo unaumwa.

Haikua shida sana niliweza kuvumilia na kufanya kazi ila bado malipo yalikua madogo na ya kuchelewa ila bado nilivumilia na kuendelea na kazi ili nipate fedha za kujikimu.

Kwa mara nyingine tena mwajili akafanya mabadiliko na kupunguza walimu nikawa mmoja ya waliopunguzwa na kirudi nyumba kukaa bila ya kazi.

Nilianza safari ya kitafuta ajira bila mafanikio kwa muda mrefu nilichoka na kukata tamaa ila kwa msaada wa makongamano na shughuli zangu za kujitolea na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs ) kupitia semina tulizo kuwa tunapewa nikapata nguvu ya kufanya maamuzi ya kujiajiri mimi mwenyewe.

Safari yangu ya kujiajiri niliianza mwezi wa 2, 2019. Kwa kua mi ni mwalimu nikaamua kuanzisha shule ya watoto wadogo (nursery school) mwanzo ulikua mgumu kwa kua sikua na mtaji wowote ule ila mtaji mkwabwa niliokua nao ni nia ya dhati ya kutaka kujiari hivo ilinibidi nitumie mtaji wa kifahamiana na watu na uzoefu wangu na hatimae nikapata jengo la kufundishia bila malipo yoyote.

Changamoto zilikua nyingi ila kwa kua nilishafanya maamuzi ya kujiari nikatangaza na kupata wanafunzi nane tu darasa letu halikua na viti wala nyenzo youote lilikua kama gofu tu ila bado sikukata tamaa kadri muda ulivokua unaenda watoto waliongezeka hadi mwaka unaisha nilikua na watoto 20.

Kikwanzo kingine kilikua 2020 pindi covid19 ilipotokea ikabidi tufunge shule kwa miezi 5 nikaaa nyumbani tena bila ya kazi yoyote huku wasiwasi na mawazo yakizidi juu ya hatima ya shule niliyoanzisha bado ni changa inahitaji muda wa kujitangaza na kukua ila ndio hivo imebidi tufunge kujikinga na covid19.

Baada ya miezi 5 kupita serikali iliruhusu shule kufunguliwa nami nikarudi eneo langu na kufungua tena hali ilikua mbaya kwani walirudi wanafunzi 8 tu ila sikukata tamaa nikaendelea nao hadi kufika mwisho wa mwaka wakafika 25.

Hadi leo 2021 nashukuru mungu shule yangu imeshajulikana na napata wanafunzi bila shida japo bado ni changa na mahitaji ni mengi ila ninacho jivunia ni uaminifu niliojenga kwa wazazi wananiletea watoto wao bila shida yoyote nina watoto wa kuanzia miaka 2 hadi miaka 5.

Wito wangu kwa wanawake na wasichana duniani nguvu ya kujitambua na kujiamini ni kubwa sana ianweza shida kikwazo chochote hata kama ni mlima evalist unaweza kusambaratika.

Shule yangu inaitwa taqwa nursery school instagram page @taqwa_school

~
Photo credit: Images provided by the storyteller.

[embed]https://sayitforward.org/wp-content/uploads/gravity_forms/1-cf117b3a3fa077f5e8b6efda923514fe/2021/10/66849AC1-08B0-4486-9A4D-4CF31FF8E19A.MOV[/embed]

Story shared by...

Shella Salum